VYAKULA VYA KUEPUKA UKIWA NA GOUT
Chakula Cha Kukwepa Ukiwa Na Gout Gout ni ugonjwa unaosababisha maumivu makali ya maungio ya mifuapa (joints). Gout huleta hushambulia joint moja au zaidi, lakini mara nyigni hutokea miguuni. Mashambulizi hutokea wakati uric acid inapoganda na kujijenga kwenye joints. Uric acid, ambayo ni antioxidant inayolinda utando wa ndani wa mishipa ya damu, huzalishwa mwilini wakati chakula cha kundi la purines kikivunjwavunjwa. Kupata au kutopata gout kunategemea zaidi urithi. Mabadiliko katika namna ya kuishi yanaweza kuzuia maumivu. Kuwa mwangalifu na vitu unavyokula na kuacha kula chakula chenye purines kwa wingi kunaweza kukuondolea dalili za gout. Nyama Zinazoleta Gout Nyama za viungo zinatakiwa kuachwa kabisa kama una ugonjwa wa gout kwa sababu zina viwango vikubwa vya purines. Nyama hizo za viungo ni kama: maini, kongosho za ndama au kondoo, figo, ubongo, na utumbo unaoliwa. Nyama nyingine zote zinatakiwa kuliwa kwa kiasi, kiasi kisichozidi wakia...