𝗝𝗜𝗡𝗦𝗜 𝗬𝗔 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗞𝗜𝗡𝗚𝗔 𝗡𝗔 𝗙𝗔𝗡𝗚𝗔𝗦𝗜 𝗦𝗘𝗛𝗘𝗠𝗨 𝗭𝗔 𝗦𝗜𝗥𝗜.(VAGINAL CANDIDIASIS)
Fangasi zinaweza kuzuiliwa kwa kiasi kikubwa na ni endapo tu mtu mwenyewe ukiamua kujilinda.Fanya yafuatayo ili kujiepusha na fangasi
1) ACHA KUPIGA UKE DEKI: nawakumbusheni tena kinadada mnafikiri kwamba ili kujiweka msafi sehemu za siri ni lazima UINGIZE KIDOLE UKENI. Mimi nawaambia ukweli na naomba mnielewe kwamba UKE unajisafishaga wenyewe na huna haja kupiga deki kwani ukipiga deki utakua umeharibu ulinzi Wa uke wako na ukishaharibu ulinzi huo unakua rahisi kupata fangasi na ndo kwanza utanuka uke kama ulikua hujui.
2) Acha matumizi ya madawa kiholela hasa dawa za UTI,kikohozi ,tumbo nk ,dawa hizo ni kama flagly,amoksilini,cipro nk.matumizi holela ya dawa hizi husababisha uharibifu Wa ulinzi Wa uke ambapo kunawaachia mwanya fangasi kushamiri.
3) usivae nguo za ndani ambazo ni mbichi au hazijakauka vizuri. Nguo za ndani zianikwe nje na zipasiwe vizuri.
4) acha kutumia sexy toys ya aina yeyote Kama dildo,acha kupiga punyeto kwa ndizi,karoti,biringanya nk
5) Punguza unene.punguza kilo zako angalau kwa asilimia 10.
6) Acha ngono zembe
7) acha kushea nguo za ndani
Kuna dalili nyingi zinazoonyesha kuwa una dalili za kua na fangasi ukeni kama zifuatazo;
1.Kuwa na miwasho sehemu za siri mara kwa mara
2.Vipele vidogo vidogo ukeni
3.Kutokwa na uchafu mweupe au wa rangi ya kijivu ukeni wenye harufu mbaya
4.Vidonda au kuwa na michubuko ukeni
5.Kutokwa na harufu mbaya ukeni
6.Kupatwa na maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.
7.Kuvimba au kuwa mwekundu katika mdomo wa nje ya uke.
8.Kuwaka moto ndani na nje ya uke.
MUHIMU
KAMA UNAPATA FANGASI ZA MARA MARA NAKUOMBA PIMA YAFUATAYO
1) KISUKARI
2) HIV NK
Ikumbukwe pia fangasi wakati Wa ujauzito inaweza kusababisha mimba kutoka au kujifungua kabla ya muda. Chukua hatua mapema.
Asanteni ;
shirikisheni na akina Dada/wanawake wengine
*Nawapenda*
@𝐃𝐫_𝐄𝐯𝐢𝐭𝐮𝐬
Comments
Post a Comment