VYAKULA VYA KUEPUKA UKIWA NA GOUT
Chakula Cha Kukwepa Ukiwa Na Gout
Gout ni ugonjwa unaosababisha maumivu makali ya maungio ya mifuapa (joints). Gout huleta hushambulia joint moja au zaidi, lakini mara nyigni hutokea miguuni. Mashambulizi hutokea wakati uric acid inapoganda na kujijenga kwenye joints. Uric acid, ambayo ni antioxidant inayolinda utando wa ndani wa mishipa ya damu, huzalishwa mwilini wakati chakula cha kundi la purines kikivunjwavunjwa. Kupata au kutopata gout kunategemea zaidi urithi. Mabadiliko katika namna ya kuishi yanaweza kuzuia maumivu. Kuwa mwangalifu na vitu unavyokula na kuacha kula chakula chenye purines kwa wingi kunaweza kukuondolea dalili za gout.
Nyama Zinazoleta Gout
Nyama za viungo zinatakiwa kuachwa kabisa kama una ugonjwa wa gout kwa sababu zina viwango vikubwa vya purines. Nyama hizo za viungo ni kama: maini, kongosho za ndama au kondoo, figo, ubongo, na utumbo unaoliwa. Nyama nyingine zote zinatakiwa kuliwa kwa kiasi, kiasi kisichozidi wakia (ounce) 4, sasawa na ukinunua robo kilo na ukaigawanya mara mbili.
Nyama zifuatazo zinatakiwa kUliwa kidogo:
. nyama ya nguruwe
. nyama ya kuku
. nyama ya bata
. nyama ya bata bukini
. nyama ya sungura
. nyama ya kondoo
. nyama ya ndama
. nyama ya paa
Chakula kinachotoka na wanyama kama mchuzi, supu ya kuku, vile vile vina purines kwa wingi.
Samaki Na Chakula Cha Bahari Wanaoleta Gout
Samaki na chakula cha baharini ni vyanzo vya purines vinavyoeleweka. Samaki wabaya kabisa kwa kuleta gout ni kama samaki wa scallops, sadini (sardines), heringi (herring), aina ya dagaa wa maji chumvi (anchovies) na samaki wa aina ya bangala (mackerel).
Samaki wengine wenye purines kwa kiwango cha kiasi ni:
. jodari (tuna)
. kambare mamba au kamongo wa maji baridi (carp)
. chewa (codfish)
. halibati (halibut)
. sangara (perch)
. samoni (salmon)
. snapper
. trout
Chakula cha baharini kama chaza, kambamti (kambakoche), kaa, na uduvi nacho kinatakiwa kuliwa kidogo kwa sababu kina purines kwa wingi.
Pombe
Bia (beer) ina purines, na hamila inayotumika kwa pombe ndiyo haswa yenye purines kwa wingi. Utafiti umeonyesha kuwa kunywa pombe ukiwa una maumivu ya gout, huongeza ukali wa maumivu hayo.
Pamoja na kwamba pombe za aina nyingine zinaweza kuwa na purines kidogo, zinaweza kuongeza kasi ya uzalishaji wa purines mwilini. Hali hiyo inaweza kuongeza kiwango cha purines ndani ya mwili. Matumizi makubwa ya pombe yanaweza kuongeza yamkini ya kushambuliwa na gout.
Katika mada nyingine tutauzungumzia ugonjwa wa rheumatoid arthritis. Usisite kutoa mchango wako wa mawazo au kuuliza maswali kuhusu mada hii.
๐๐ฌ๐ ๐ช๐จ๐๐๐ช๐ก๐ ๐ฏ๐๐๐๐ ๐ช๐ฃ๐๐ฌ๐๐ฏ๐ ๐ฌ๐๐จ๐๐ก๐๐๐ฃ๐ ๐ฃ๐๐ข๐ ๐ ๐ช๐ฅ๐๐ฉ๐๐ ๐๐๐ง๐ช๐ ๐ฅ๐๐ฅ๐ ๐๐๐ drevitusnaafya@gmail.com ๐๐ ๐ ๐ช๐ฅ๐๐ฉ๐๐ ๐จ๐๐ข๐ช ๐ฃ๐๐ข๐๐ +255768892003




Comments
Post a Comment