KUJAA MAJI KWENYEGOTI/KNEEL EFFUSION.
Maji Kwenye Goti Ni Tatizo Gani? Maji kwenye goti (knee effusion au water on the knee) ni hali ya kupata maumivu makali kutokana na maji kujaa kuzunguka au ndani ya maungio ya mifupa ya kwenye goti (knee joint). Hali hii ikitokea, kujua chanzo na dalili zake na njia bora ya kuyaondoa maji hayo kwenye goti ni kitu muhimu. Njia utakayoitumia kuuondoa uvimbe huu itategemea chanzo cha uvimbe na daktari anaweza kuhitajika kufanya uchunguzi. Kiasi kidogo cha maji huwepo kwenye joint ya kawaida. Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 27 ya watu hupata tatizo la maji kwenye magoti kwa muda fulani. Umbile La Goti Goti ni jointi iliyo kubwa na yenye sehemu nyingi kuliko jointi zote katika mwili. Jointi ya goti huunganisha mfupa wa paja (femur) na mfupa wa chini ya goti (tibia). Mfupa mdogo unaokwenda sambamba na mfupa wa chini ya goti (fibula) na kifuu cha goti (patella) ni mifupa mingine inayojenga jointi ya goti. Tendoni huiunganisha mifupa ya goti na misuli ya m...